Monday, February 13, 2012

BONGO MOVIE NDANI YA TMES FM
Bongo Movie club juzi kati waliivamia Redio ya Time Fm na kufanya shoo ya nguvu sana watangazaji wetu walikuwa Masanja Mkandamizaji pamoja Steve Nyerere,Dhumuni lilikuwa ni kuwachangisha wadau wakubwa wa tasnia ya movie kwa ajili ya wenzetu waliopatwa na mafuriko makubwa pale Jangwani,tuliguswa sana na maafa hayo na ndio maana tukasukumwa kufanya jambo ilo kwani watu wengi wanaonunua kazi zetu ni watu wa hali chini sana kwa asilimia 70 kama sikosei,Sasa ni jukumu letu sisi kwarudisha shukrani zetu dhati kwa kujitolea kufanaya tukio ilo pia leo usikose kuja pale Uwanja mpya wa Taifa kuna mechi kali kati ya Bongo movie na Wanamuziki wa Dance kiingilio ni shilingi alfu mbili tu pesa zote zitazopatikana zitaenda kwa ndugu zetu waliopatwa na maafa hayo
Masanja akiwa kazini kuendesha zoezi ilo kulia Mkoloni mwanamuziki wa kizazi kipya kma mnakumbuka walikuwa na kundi lililokuwa likiitwa Wagosi wa Kaya
Mainda na Steve Nyerere

Mambo yakiendelea.....

Chopa Mchopanga naye alikuwepo katika zoezi ilo

Davina mrembo wa Bongo Movie

Mainda mwanadada machachari katika fani ya uigizizaji, Yeye ni mwanakamati mkuu katika swala zima la ushagiliaji pale Uwanja wa Taifa ni sipakukosa

Wanabongo Movie wakiwepo ndani ya mjengo wa Times Fm

 Dada Heriety Chumila mwanabongo movie, Yeye pia alipatwa na mafuriko na kupoteza kila kitu na kuanza upya naye alikuwepo kuwawakilisha wanzake wote waliopatwa na janga ilo

Karibu Uwanja wa Taifa kuona mechi kali .

Thursday, February 2, 2012

BONGO MOVIES VS WANAMZIKI WA DANSI KUKIPIGA JUMAPILI KUCHANGIA WAATHILIKA WA MAFULIKO
katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Compact Media Company, Eliya Mjatt Timu meneja wa timu ya wanamziki wa dansi, Mwijuma Muhumini 'Kocha wa Dunia' (kushoto) wakizungumza na wahandishi wa habari, Dar es salaam leo kuhusu mechi yao ya hisani na wachekeshaji na waigizaji 'Bongo Movies' kwa ajili ya kuchangia waathilika wa mafuriko, utakaofanyika jumapili katika uwanja wa taifa kulia ni Kocha mchezaji wa timu ya 'Bongo Movies' Chiki Mchoma