Sunday, January 22, 2012

NEW YORK YADATA NA MZEE YUSUF
Mfalme wa mipasho, Mzee wa kulambisha akipagawisha Mont Vernon, New York kwenye Show kabambe Jumamosi Janauary 21, 2012 iliyokonga nyoyo za mashabiki kwa kuimba nyimbo zake kwa ustadi mkubwa huku akiwa mcheshi muda wote.
Juu na chini ni Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York.
Kulia ni Balozi wa Somalia Umoja wa Mataifa Mh. Dr.Elmi Ahmed Dualeh akiwa na mke wake wakipiga picha ya pamoja na Mzee Yusuf (kati), Mh. Dr. Elmi Ahmed Dualeh alishawahi ishi Zanzibar miaka ya nyuma wakati Mzee Yusuf alipokua mdogo.
Mzee wa alamba, Haaam, Haaam akifanya makamuzi New York.
Mashabiki waliokuja kulambishwa wakichenguka na huku wakimtunza Mzee Yusuf aliyekonga nyoyo zao kwa show iliyofana iliyofanyikia Mont Vernon, New York, Nchini Marekani.
Juu na chini mashabiki wa New York na Vitongoji vya jirani wakiendelea kulambishwa na Mzee Yusuf.

Ilikua balaa hakuna kukaa chini Mzee wa Alamba, Mfalme wa mipasho alivyofunika New York.
Mashabiki wakiimba pamoja na Mzee Yusuf
Ilikua si mchezo uliyekosa karibu DC Feb 4 atalambisha mashabiki wa DMV.
Mashabiki wa New York na Vitongoji vyake wakipagawika na Mzee Yusuf, Mfalme wa mipasho.
Mashabiki wakilambishwa na Mzee Yusuf alipofanya show Mjini New York Jumamosi January 21, 2012

Tuesday, January 17, 2012


 ONYESHO LA LADY IN RED 2012 KUITIKISA DAR
Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous akitoa maelekezo kwa wabunifu wenzake wa mavazi na wanamitindo watakaoshiriki katika onyesho la Lady in Red 2012 Reloaded linalotarajiwa kufanyika Februari 2, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Onyesho hilo linatarajiwa kuwakutanisha wabunifu wapatao 20 ambao wataonyesha mavazi yao.

Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous (wa pili kulia) wa Fabak Fashion ambaye pia ni muandaaji wa onyesho la Lady and Red akiwa pamoja na wabunifu wenzake wa mavazi na wanamitindo watakaoshiriki katika onyesho la Lady in Red 2012 Reloaded linalotarajiwa kufanyika Februari 2, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Onyesho hilo linatarajiwa kuwakutanisha wabunifu wapatao 25 ambao wataonyesha mavazi yao.


Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous (wa pili kushoto) akiwa pamoja na wabunifu wenzake wa mavazi watakaoshiriki katika onyesho la Lady in Red 2012 Reloaded linalotarajiwa kufanyika Februari 2, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 


Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous (wa tatu kulia) akiwa pamoja na wabunifu wenzake wa mavazi watakaoshiriki katika onyesho la Lady in Red 2012 Reloaded linalotarajiwa kufanyika Februari 2, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 


Mmoja ya wabunifu wa mavazi akimpima Mwanamitindo watakaoshiriki katika onyesho la Lady in Red 2012 Reloaded linalotarajiwa kufanyika Februari 2, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous (wa tatu kushoto) akiwa pamoja na wanamitindo watakaoshiriki katika onyesho la Lady in Red 2012 Reloaded linalotarajiwa kufanyika Februari 2, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 


Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous (wa pili kushoto) akiwa pamoja na wabunifu wa mavazi watakaoshiriki kwa mara ya kwanza katika onyesho la Lady in Red 2012 Reloaded linalotarajiwa kufanyika Februari 2, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous akiwa pamoja na wabunifu wenzake wa mavazi na wanamitindo watakaoshiriki katika onyesho la Lady in Red 2012 Reloaded linalotarajiwa kufanyika Februari 2, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 





Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous akiwa na mbunifu mwenzake Gymkhana Hilali a.k.a Paka Wear pamoja na wanamitindo watakaoshiriki katika onyesho la Lady in Red 2012 Reloaded linalotarajiwa kufanyika Februari 2, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Onyesho hilo linatarajiwa kuwakutanisha wabunifu wapatao 20 ambao wataonyesha mavazi yao.

Mbunifu wa mavazi Gymkhana Hilali a.k.a Paka Wear akiongea na wanamtindo watakaoshiriki katika onyesho la Lady in Red 2012 Reloaded linalotarajiwa kufanyika Februari 2, 2011 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Onyesho hilo linatarajiwa kuwakutanisha wabunifu wapatao 20 ambao wataonyesha mavazi yao. (Picha zote na C. A. Kajuna,www.kajunason.blogspot.com)



Thursday, January 12, 2012

JAMES KIBOSHO AZIBA PENGO LA CHAZ BABA TWANGA ,DOGO RAMA, VANANCE, JUMANNE WAFUKIA MASHIMO

MPIGA ngoma nguli wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta', James Kibosho, amerithi mikoba ya aliyekuwa mwimbaji wa bendi hiyo, Charles Gabriel 'Chaz Baba' aliyetangaza kujiengua wiki hii na kuhamia Mashujaa Musica.

Mmoja wa wanamuziki galacha wa Twanga Pepeta, Khamis Kayumbu 'Amigolas' jana usiku wakati wa onesho la Twanga Pepeta kwenye ukumbi wa Club Bilicanas, alimtangaza Kibosho kuwa ndiye kiongozi wa kupanga muziki jukwaani (Stage Master), nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Chaz Baba.

Tangazo hilo la Amigolas lilipokewa kwa hoi hoi, nderemo na vifijo kutoka kwa mashabiki kochokocho wa Twanga Pepeta waliojaa pomoni ukumbini hapo kushuhudia burudani ambayo pia ilishuhudiwa na mwimbaji wa bendi ya Mapacha Watatu, Kalala Hamza 'Junior', Meneja wake, Hamisi Dacorta na wanamuziki wengine wa FM Academia, Patcho Mwamba na Pablo Masai.

Waimbaji wa Twanga Pepeta, Ramadhan Athuman 'Dogo Rama', Venance Mgori na rapa na mwimbaji, Jumanne Said, wakiongozwa na kiongozi msaidizi wa bendi hiyo, Saleh Kupaza, walidhihirisha hakuna pengo lililoachwa na Chaz Baba kutokana na kuimba kwa ufasaha, 'vipande' alivyokuwa akiimba.

Wanamuziki wengine wa Twanga Pepeta waliokuwa jukwaani kuongoza mashambulizi ni kiongozi mkuu, Luiza Mbutu, Amigolas, Haji Ramadhan (mshindi wa BSS 2011), Mwinjuma Muumin, Janeth Isinika, Khadija Mnoga 'Kimobitel', Grayson Semsekwa na Msafiri Said 'Diouf'.

Pia walikuwepo wapiga vyombo, Miraji Shakashia 'Shakazulu', Jojoo Jumanne, Godfrey Kanuti, Selemani Shaibu, Victor Nkambi na Hassan Kado. Wanenguaji ni Asha Said 'Sharapova', Maria Soloma, Betty Johnson 'Baby Tall', Mary Khamis na wengineo.

Twanga Pepeta hivi sasa inatamba na albamu yake ya 11 ya Dunia Daraja yenye nyimbo za Kauli, Kiapo cha 
Mapenzi, Umenivika Umasikini, Mtoto wa Mwisho, Dunia Daraja na Penzi la Shemeji.

Albamu zilizopita za bendi hiyo ni Kisa cha Mpemba (1999), Jirani (2000), Fainali Uzeeni (2001), Chuki Binafsi (2002), Ukubwa Jiwe (2003), Mtu Pesa (2004), Safari 2005 (2005), Password (2006), Mtaa wa Kwanza (2007) na Mwana Dar es Salaam (2009).

Muandishi: MICHUZI JR 
HEY LADIES PENDEZA NA
CHEEKS FASHION 

Tumeshusha mzigo mpya kwa "Ladies".

Pamba za kutosha, hand bag pomba, viatu vikali, chain za kufa mtu, saa zilizoenda shule, nguo za ndani  zenye mvuto n.kMapigo ya kisasa kwa wewe dada, mama, mtoto..
Njoo tupendeze. Utakutana na wapendao kuwa smart katika duka letu.

Tunapatikana
Kinondoni, Manyanya, opp Togo, Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 713 55 84 94

Barua pepe: villa_sarafina@yahoo.com
Blogu: www.rumaafrica.blogspot.com






















GRAPHIC DESIGNER: 
Rulea Sanga | www.rumaafrica.blogspot.com | rumatz2011@yahoo.com | 
+255 715 85 15  23
WAOHHH!!!.....CHEEKS FASHION

Tumeshusha mzigo mpya kwa "Ladies".

Pamba za kutosha, hand bag pomba, viatu vikali, chain za kufa mtu, saa zilizoenda shule, nguo za ndani zenye mvuto n.k

Mapigo ya kisasa kwa wewe dada, mama, mtoto..
Njoo tupendeze. Utakutana na wapendao kuwa smart katika duka letu.






POA TUONANE CHEEKS FASHION














GRAPHIC DESIGNER: Rulea Sanga | +255 715 85 15 23 | rumatz2011@yahoo.com