Siku
ya jana ya Jumamosi kulikuwa na maafali
ya kwanza ya wanafunzi waliokuwa
wanahitimu mafunzo ya ushonaji katika chuo
cha NEW DAY AFRICA FOUNDATION kilichopo Tegeta
Kibaoni jijini Dar es salaam. Chuo kipo chini
ya Mkurugenzi Bi. Upendo Kilahiro na Bw. Amon Kilahiro.
Maono ya
kuanzisha NE DAY AFRICA FOUNDATION yalianza mwaka 2011 na mwaka 2013
ndipo maono haya yakazaa matunda. Upendo Kilahiro alimshukuru Mungu kwa
kutimiza ndoto zake za kuwa na kitu ambacho kinaweza kusaidia jamii
kiuchumi.
Kuna
vitu ambavyo Mungu amegawa kwa kila mtu lakini wapo wengine
wamependelewa kuwa na moyo wa upendo, Bi Upendo kilahiro ni mmojawapo wa
kuwa na zawadi ya upendo kama jina lake linavyoitwa “UPENDO”.
Bi. Upendo na mume wake Amon Kilahiro wamekuwa wakitoa mafundisho hayo ya
ushonaji bure na bila ya malipo yoyote. Wanafunzi wamekuwa wakitumia vyerehani
vyao bila ya malipo yoyote, gharama za uendeshaji kama umeme unaotumiaka
kuendesha mashine za ushonaji zimekuwa zikitolewa Wakurugenzi hao (Upendo Kilahiro na mume
wake). Kwakweli huu ni upendo wa hali ya juu ambao unahitaji kuigwa na watu
wote, kwani unaweza kufikiria jinsi maisha ya sasa yalivyoo magumu, lakini watu
hawa hawakuweza kuliangalia hilo bali waliangali sana kusaidia wale wenye
uhitaji wa kusoma na hawana pesa za kulipia mafundisho yao.
Wahitimu
walimshukuru sana Mungu kwa kuwapa mama na baba ambao ni Upendo Kilahiro na
mumwe wake Amon Kilahiro kuwafungua katika giza na kuwaweka katika nuru ya
mafanikio ya kimaisha. Elimu waliyopata sio elimu ya theory bali ni elimu ya
vitendo.
Wahitimu walionekana kuwa na
sura za huruma wakati kumuaga Upendo Kilahiro na mwalimu wao kwani
walisema wanatamani kuwa naye siku zote , na hii ni kwasababu ya upendo
waliokuwa nao wakati wapo masomoni na wengine walioneka
kutokwa na machozi.
Kuna
baadhi ya wanafunzi waliweza kupita mbele na kueleza kile ambacho wamekipata
chuoni. Baadhi yao walisema wao walifika pale chuoni wakiwa hawajui hata
kuchomeka sindano katika mashine ya kushonea, ila baada ya kufundishwa na
mwalimu wao waliweza kujua kuchomeka sindano na kuweza kushona nguo za aina
yoyote. Wahitimu hao walisema kwa sasa wanaweza kushona mshono wowote.
Wahitimu hao
waliweza kuimba wimbo wa kumuaga Upendo Kilahiro, mwalimu wao na uongozi mzima wa chuo hicho. Wimbo
ulikuwa umejaa majonzi kutokana
yale
waliotendewa wanahitimu hao wakiwa masomo.Walisema wamejifunza mambo
mengi ya kimwili na kiroho na kubwa zaidi wamejipatia ujuzi wa ushonaji.
Mbali
ya hayo yote, Mkurugenzi Upendo Kilahiro alimshukuru sana Mungu kwa kutimiza
ndoto yake aliyokuwa nayo kwa muda mrefu ya kuweza kusaidia jamii. Kwake
anasema ni mmoja wa muujiza mkubwa Mungu amefanya katika maisha yake. Upendo
alionekana kuongea kwa hisia kali sana juu ya mafanikio aliyokuwa nayo. Amesema
mara nyingi amekuwa busy sana na kazi za kifamili, kihuduma katika kazi ya
Mungu, safari mbalimbali nje ya Tanzania kama UK na Canada kwa kazi ya Mungu na
wakati
huo huo anatakiwa kutimiza ndoto yake ya kuisadia jamii hasa suala hili la
wanafunzi wa ushonaji. Amekuwa akijibana kwa mambo mengi hasa katika suala la
pesa ili kuhakikisha hawa wanafunzi wanapata mahitaji yote ya msingi katika
suala lao la ushonaji. Wanafunzi
waliweza kuvaa sale zao ambazo wamezitengeza wenyewe na liliwemo vazi alilo vaa
Upendo Kilahiro. Wanafunzi hawa ukiangalia mavazi hao, kwa kweli utasema ni
wabunifu wa hali ya juu sana.
UPENNDO KILAHIRO alisema anajisikia kuwa mpweke sana kwa kuangana na
wanafunzi hawa kwani amekuwa akiishi nao kama familia na sio kama
wanafunzi. Ila alisema kila jambo lina mwanzo na mwisho kwahiyo hata
hawa wanafunzi wake umefika wakati wa kuondoka. aliwaomba wanafunzi
wazidi kufika chuoni hapa kama kuna jambo watakuwa wanahitaji kutoka
kwake, milango iko wazi na yeye atawasaidia bila ya kujali kuwa
wamemaliza masomo yao.
Alisema lengo lake ni kuona hawa viajana wanapata kazi zao za
kujitegemea ili waweze kuwa mchango mkubwa katika Taifa la Tanzania
kwani bado wana nguvu za kulitumikia Taifa lao. Watu kama hawa ambao
walikuwa hawana ujuzi wako wengi sana mitaani wanashindwa watu wa
kuwainua ili wasimame wenyewe, alisema.
-------------------------------------
Katika
hotuba yake, alikuwa na haya machace ya kusema:
NEW DAY AFRICA FOUNDATION (NEDAFO)
NEW DAY AFRICA FOUNDATION (NEDAFO) ni shirika la Kikristo linatoa huduma za
kiroho na za kijamii. Shirika hili lilianza rasmi mwaka 2011 chini ya mbeba
maon Bi. Upendo Kilahiro na daadae shirika hili lilipanuka na kuongeza kwa
kusaidiwa na mumewe Bw. Amon Kilahiro hadi kupata uongozi wa
NEDAFO.
Shirika
hili lilianza hapa Tanzania lakini lina maono ya kusambaa mataifa yote ya
Afrika kwa lengo la kuwapa elimu na tumaini jipya kwa kila mmoja hasa wanawake,
wasichana na watoto.Shirika
hili lilianza miaka mitatu iliyopita lakini mwaka huu 2013 tumeanza kutoa
huduma za kijamii. NEDAFO imeweza kutoa mafunzo ya ushonaji kwa wanawake na
wasichana, nah ii ni sehemu tu ya mengi
ambayo NEDAFO inamtumainia Mungu kutuwezesha kuyafanya katika siku za
usoni ili kufikia lengo la maono tuliyonayo.Shirika
hili limekuwa likiwafundisha wanafunzi bure na Mkurugenzi amekuwa akiwajibika
kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora, vitendea kazi vya kisasa vinakuwepo,
ma pia kuhakikisha wanafunzi wanakuwa katika maadili yale Mungu anahitaji kwa
kila mwanadamu kuwa nayo.UTENDAJI
NEDAFO inafanya kazi ya kuwaendeleza wale wenye uhitaji wa kujiendeleza ili
waweze kujikimu katika maisha, kujisimamia kujiajiri na kuweza kuwasaidia
wengine kwa yale waliojifunza katika shirika hili la NEDAFOWASILIANA NASI KWA SIMU
+255 757 578114
www.upendokilahiro.blogspot.com
MUNGU AKUBARIKITUONE YALIYOTOKEA

Mkurugenzi wa New Day Africa Foundation, Bi. Upendo Kilahiro

Upendo Kilahiro
Mkurugenzi wa New Day Africa Foundation, Bi. Upendo Kilahiro akiwa na baba yake ambaye alikuwa mgawaji wa vyeti siku hii
Mkurugenzi wa New Day Africa Foundation, Bi. Upendo Kilahiro akiwa na
furaha ya ajabu kutimiza ndoto yake, Vazi alilovaa limebuniwa na
wanafunzi wake.
Mkurugenzi wa New Day Africa Foundation, Bi. Upendo Kilahiro
akimshukuru Mungu kwa kumuwezesha kufika pale alipokuwa akiota kila siku
kupafikia.
Hapa ni nyumbani kwa Upendo Kilahiro Tegeta Kibaoni
Mpambaji akiwa kazini kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
..mmoja wa viongozi wa juu katika New Day Africa Foundation akiwa na furaha ya ajabu
Wa pili kutoka kulia na mama na Upendo Kilahilo na anayefuatia ni baba na upendo Kilahilo wakiwa katika picha ya pamoja.
Wahitimu wa chuo cha NEW DAY AFRICA FOUNDATION (NEDAFO) wakiwa katika picha ya pamoja.
Mavazi haya waliyovaa hawa wahitimu yamebuniwa na wao wenyewe.
Huu ni uongozi wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION (NEDAFO)
Wahitimu wakiwa wamejiaandaa kupokea vyeti vya kuhitimu
Wahitimu wakionyesha mishono ya mavazi yao waliyoibuni wakiwa chuoni
Kulia ni mtoto wa Upendo Kilahiro ambaye naye amejifunza kushona nguo kwa kutumia mashine za kisasa zilizopo hapo chuoni. Hapa akionekana akisali wakati wa kuombea chakula na vinjwaji
Wahitimu wakiwa katika sala ya kuombea vinywaji na chakula
Mkurungenzi wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION, Upendo Kilahiro akijitambulisha
Mwalimu wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION akijitambulisha
Mkurugenzi wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION Upendo Kilahiro akiongea na wahitimu
Mkurugenzi wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION akiita majina ya wahitimu kuchukua vyeti vyao vya kumaliza mafunzo ya ushonaji.
Wahitimu wakionysha vyeti vya vya ushindi kumaliza masomo yao ya ushonaji.
Mwalimu akiwa na wahitimu wakiimba wimbo wa kuagana na uongozi mzima wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION